Jumanne 6 Mei 2025 - 12:46
Je, mfumo wa Hawza ya Najaf ulikuwa ni wenye kujiepusha na siasa?

Kinyume na dhana iliyojengeka, maktaba ya Najaf hayajawahi kujitenga na siasa, bali katika historia yake imekuwa na nafasi muhimu katika mageuzi ya kisiasa. Kuanzia ushiriki wake katika harakati za mashruta na mapambano dhidi ya ukoloni, hadi fatwa ya jihadi ya Ayatullah Sistani dhidi ya Daesh (ISIS), yote haya yanaonyesha muunganiko wa kina wa hawza hii na siasa. Kulinganisha hawza ya Najaf na Qom huku ukitarajia utendaji sawa si sahihi, kwa sababu mazingira ya kijamii na kisiasa ya nchi hizi mbili ni tofauti.

Kwa mujibu wa ripoti ya  Shirika la Habari la Hawza, Hawza ya Najaf, kama mojawapo ya vituo muhimu zaidi vya kielimu na kidini katika ulimwengu wa Kishia, daima imekuwa na mchango katika mabadiliko ya kijamii na kisiasa. Pamoja na kuwepo kwa vikwazo vya kihistoria, kuanzia katika kipindi cha mashruta hadi mapambano dhidi ya Daesh, daima imekuwa na uhusiano wa karibu na siasa. Kwa muktadha huu, tutaangazia swali na jibu kuhusu mada hii kama ifuatavyo:

Swali:
Je, maktaba ya Najaf, ambayo sifa yake kuu ni kujiepusha na siasa, leo hii yanaweza kuwa kigezo bora kwa hawza nyingine, kwa maana ya kutokujihusisha na serikali huku ikitimiza majukumu yake, na hivyo isihusishwe na matatizo au mapungufu yoyote?

Jawabu:
1. Dhana kwamba kujiepusha na siasa ni sifa kuu ya maktaba ya Najaf si sahihi. Haiwezekani kuielewa hawza yeyote bila ya kuihusisha na mijadala ya kisiasa, na hawza ya Najaf haikuwa nje ya mfumo huu.

Kwa sababu hiyo, hawza hii kama zilivyo hawza nyingi kwenye ulimwengu wa Kiislamu, hasa katika kipindi cha zaidi ya karne moja iliyopita, imekuwa na athari katika mazingira ya kisiasa katika ulimwengu wa Kiislamu. Hili halina maana kwamba ndani ya hawza hii hakujakuwepo mitazamo isiyopendelea kushiriki katika siasa, kwa kuwa fikra kama hizi hata katika Hawza ya Qom (ambayo ni chimbuko la Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran) pia ipo Baadhi ya mitazamo ya kihafidhina, licha ya kukubali kuwepo kwa uhusiano kati ya dini na siasa, kwa sababu mbalimbali, haiko tayari kujihusisha na masuala ya kisiasa.

Msingi wa Hawza ya Najaf, kwa kuzingatia misingi ya kifikra na imani, daima umekuwa ni kuamini katika ulazima wa dini kushiriki katika siasa, na kimatendo pia imekuwa ikishiriki. Kwa mfano, katika harakati za mashruta nchini Iran, hawza hii ilikuwa na nafasi muhimu, na marehemu Akhund Khurasani alichukua jukumu muhimu katika jambo hilo, kiasi cha kwamba baada ya kuona mwelekeo wa mashruta unaenda kinyume, aliamua kuja Iran kushiriki moja kwa moja katika mchakato huo. Hata hivyo, kutokana na kifo chake cha ghafla, jambo hilo halikutimia.

Baada ya kipindi hicho, Hawza ya Najaf iliendelea kuwa na ushawishi katika matukio mbalimbali ya Iran na Iraq, yakiwemo mapambano dhidi ya ukoloni na harakati ya mwaka 1920 ya watu wa Iraq dhidi ya Uingereza. Hawza ya Najaf, pamoja na hawza nyingine za Iraq, zilikuwa na nafasi ya umuhimu mkubwa kiasi kwamba maandalizi ya harakati hiyo yalianza mwaka 1917 huko Najaf kwa jina la "Mapinduzi ya Najaf", na baadaye ikaenea nchi nzima hadi kufikia harakati ya mwaka 1920 dhidi ya wavamizi, chini ya uongozi wa marehemu Mirza Muhammad Taqi Shirazi, aliyekuwa mkuu wa Hawza ya Najaf. Baada yake, marehemu Shari’at Isfahani aliendeleza njia hiyo ya kupambana na ukoloni.

Katika zama za sasa pia, ingawa baadhi wamekuza mtazamo uitwao "maktaba ya Najaf" na kuihusisha na kujiepusha na siasa, ukweli ni kwamba haiwezekani kuutaja mfumo wa Hawza ya Najaf kuwa hauna mwelekeo wa kisiasa au hujiepusha na siasa. Ikiwa mazingira na hali zingekuwa tayari kuruhusu ushiriki wa hawza na wanazuoni katika siasa, basi Iraq ingekuwa katika hali tofauti kabisa na ya sasa.

Katika kipindi cha utawala wa Baath nchini Iraq, kutokana na ukandamizaji mkubwa, Hawza ya Najaf haikuwa na fursa ya kufanya harakati, kama ilivyokuwa Iran wakati wa Reza Khan.

Harakati ndogo za kisiasa hazikuvumiliwa na utawala wa Baath, na kwa sababu hiyo, Ayatullah Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr pamoja na makundi ya wanazuoni kutoka katika familia za Hakeem, Sadr, Shahrudi, na wengineo waliuawa kishahidi.

Hii inaonyesha kwamba: Kwanza, Hawza ya Najaf hata katika kipindi cha udhibiti mkali kutoka katika utawala wa Baath haikujiyenga na siasa; pili, mashinikizo yaliyokuwepo yalizuia kabisa uwezekano wa harakati. Kama kungekuwa na fursa hata ndogo ya shughuli za kisiasa, bila shaka hawza hii ingezitimiza wajibu wake wa kisheria kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa.

Ushahidi wa jambo hili ni harakati ya "Intifadha ya Sha’baniyya" katika kipindi cha utawala wa Baath, chini ya uongozi wa marehemu Ayatullah al-Udhma Khou’i (r.a). Katika harakati hii, wananchi wa Iraq wakiongozwa na marjaa huyu mkubwa waliinuka na hata kudhibiti baadhi ya mikoa. Kutokana na hilo, marehemu Ayatullah Khou’i aliteua mabaraza ya kusimamia maeneo hayo. Ingawa harakati hiyo ilizimwa kwa ukatili, hatua aliyoichukua inaonyesha kwamba Ayatullah Khou’i, aliyekuwa mwanazuoni mashuhuri wa Hawza ya Najaf, licha ya kuwa na misingi ya nadharia ya Wilayat al-Faqih, pia kwa vitendo alitumia mamlaka hiyo pale mazingira yaliporuhusu.

Baada ya kufariki kwa Ayatullah Khou’i, Hawza ya Najaf ilibaki chini ya uongozi wa marjaa wakubwa, akiwemo Ayatullah al-Udhma Sayyid Sistani, ambaye baada ya kuanguka kwa utawala wa Baath, aligeuka kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Iraq. Fatwa na maelekezo yake yalikuwa na athari ya moja kwa moja katika mwelekeo wa kisiasa na kijamii kwa watu wa Iraq.

Fatwa yake ya jihadi dhidi ya Daesh ilichochea harakati za wananchi kupambana na kundi hilo, na ilikuwa mwanzo wa kuanzishwa kwa kikundi cha "Hashd al-Sha’bi" nchini Iraq, kikundi kilichochangia pakubwa katika kutatua mgogoro wa Daesh.

Ayatullah Sistani, kama kiongozi wa kisiasa, hupokea ujumbe wa ngazi za juu za kidiplomasia na hutoa maoni kuhusu masuala muhimu ya Iraq. Msimamo huu ni uthibitisho wa kutumia mamlaka ya kidini ambayo kwa mujibu wa mafundisho ya Kishia, wanazuoni wenye sifa kamili hupewa, na wanapaswa kuitumia pale mazingira yanapowaruhusu.

Mbali na haya, kama inavyojulikana, baadhi ya wanahawza wa Najaf wanashiriki moja kwa moja katika siasa, kwa mfano kupitia kuunda vyama na kushiriki katika chaguzi za bunge, ambazo hupelekea uteuzi wa viongozi wa serikali. Hadi sasa, Ayatullah Sistani hajawahi kupinga shughuli hizi. Mbali na yeye, marjaa wengine wakubwa wa Najaf pia wamekuwa wakitoa misimamo kuhusu masuala ya kisiasa na kijamii, jambo linaloonyesha wazi kwa wanauamini uhusiano wa kimsingi kati ya dini na siasa.

2. Kudai kuwa kutokujihusisha na serikali ndicho kigezo cha ubora wa maktaba ya Najaf ni matokeo ya kutokuelewa wajibu wa hawza na wanazuoni kuhusu serikali ya Kiislamu na uundwaji wake. Je, hawza na wanazuoni hawana wajibu wowote kuhusu kuasisiwa kwa serikali ya Kiislamu iwapo mazingira yameruhusu na wananchi wameunga mkono? Je, wajibu wao ni kuwa pembeni ya serikali bila kujali asili yake? Je, kigezo hiki kimetokana na mafundisho yapi ya Kiislamu, na ni ipi kauli ya kifiqhi au kisheria inayoonesha kuwa hawza na wanazuoni hawapaswi kushiriki katika uundaji wa serikali wanapoweza kufanya hivyo?

3. Kwa jumla, kulinganisha hawza ya Najaf na Qom na kudhani kuwa mazingira ya kijamii na kisiasa ya nchi hizi mbili ni sawa na hivyo kutarajia utendaji sawa, si sahihi. Ushawishi wa Hawza ya Najaf, kwa kuzingatia kutokuwepo kwa mazingira ya kuanzisha serikali ya Kiislamu, umekuwa na jitihada katika kutekeleza hukumu za Kiislamu kwa kadiri iwezekanavyo. Hali hii ni tofauti kabisa na Qom ambayo, chini ya mfumo wa Kiislamu, ina mazingira yanayoruhusu kushiriki katika kuiongoza jamii, na kutotumia mazingira hayo ni sawa na kukana juhudi na jitihada za kihistoria za wanazuoni kwa ajili ya utekelezaji wa hukumu za Kiislamu.

4. Baadhi ya watu, kwa sababu ya kuowanisha matatizo na kushindwa kwa serikali na dini au hawza, na athari mbaya katika imani ya watu kuhusu dini, huwasilisha mtindo wa Najaf kuwa kama ndio kigezo bora. Jibu kwa hoja hii limetolewa mahala pake, na sisi pia tumelielezea.

Chanzo: Kituo cha Utafiti na Majibu kwa Shubha (Hawza)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha